- Anicent Oura dakika ya 33 anafunga goli la kuongoza kwa mnyama ugenini
- James Mwashinga anafunga goli la usawa kwa wenyeji dakika ya 36
- Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC kwenye Ligi Kuu baada ya dakika 45.
- Je Mnyama atatoboa and Pamba Jiji atauchukua mchezo?
Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC dakika 45 za mwanzo Uwanja wa CCM Kirumba. Anicent Oura alifunga goli la kuongoza dakika ya 33. Dakika 3 mbele Pamba Jiji FC walisawazisha kupitia kwa James Mwashinga dakika ya 36.
SOMA HII: Simba SC yajivunia ubora wa kikosi 2025/26/ Fixture, Standings

Matukio ya halftime: Rekodi za Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC SC

| Pamba Jiji FC | Simba SC | |
| 3 | Mashuti | 3 |
| 3 | Lenga lango | 2 |
| 47% | Umiliki | 53% |
| 0 | Mashuti yasiyolenga lango | 1 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 0 | Kadi ya njano | 0 |
| 0 | Kona | 0 |
| 1 | Magoli | 1 |
Simba SC wameongoza umiliki, Mwishanga awaduwaza
Katika dakika 45 za mwanza wageni Simba SC wameongoza kwenye umiliki wakipiga jumla ya mashuti 3 langoni kwa Pamba Jiji FC. Katika mashuti hayo ni mawili yalilenga lango na moja kwenda nje ya lango.
Pigo la faulo ya James Mwishanga limewaduwaza Simba SC baada ya mlinda mlango kushindwa kuokoa hatari hiyo. Ndani ya dakika 45 timu zote mbili zilikwenda mapumziko zikiwa hazijapata pigo la kona wala kadi nyekundu.
Msimamo wa Pamba Jiji FC vs Simba SC
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 3.Simba SC | 13 | 8 | 4 | 1 | 28 |
| 5.Pamba Jiji FC | 16 | 6 | 7 | 3 | 25 |
Kikosi cha Pamba Jiji FC vs Simba SC
Langoni
Yona Amosi ana miaka 26 alianza langoni kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba SC. Alikuwa imara langoni kwa kuokoa hatari mbili langoni mbele ya Simba SC. Mlinda mlango huyu ni raia wa Tanzania.
Mabeki
Abdulmajid Mangalo,Ibrahim Abrahim, Keneth Kunambi na Hussen Kibailo hawa waliongoza safu ya ulinzi kwenye mchezo dhidi ya Simba SC. Nyota hawa walihakikisha kiungo tegemo wa Simba SC, Clatous Chama haleti hatari kubwa katika lango.
Viungo
Sharpahn Sawa, Mathew Tegisi na Michael Samamba hawa ni viungo walioanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wakimkabili mnyama. Sawa ni raia wa Kenya ni kiungo muhimu kwenye timu hiyo. Tegisi yeye amesajiliwa na Pamba Jiji FC akitokea Klabu ya Shabana FC ya Kenya. Samamba ni nahodha wa Pamba Jiji FC alianza kwenye mchezo dhidi ya Simba SC.
Washambuliaji
Peter Lwasa, Zabona Mayombya na James Mwashinga. Lwasa ni raia wa Uganda aliwahi kucheza Klabu ya Kagera Sugar. Zabona Mayombya na James Mwashinga waliongoza safu ya ushambuliaji hawa waliwasumbua mabeki wa Simba SC wakiongozwa na Rushine De Reuck. James alifunga goli kwa pigo la faulo dhidi ya Simba SC.
Wachezaji wa akiba
Brian Elishahanda, Shashiri Nahimana, Amosi Kadikilo, Abdoulaye Camara, Abdallah Khamis, Denis Richard, John Ben, Henry Msabila. Elishanda ni beki raia wa Kenya alijiunga na Pamba Jiji FC akitokea Kakamega Homeboyz. Nahimana ni kiungo raia wa Burundi alitambulishwa hapo akitokea Bandari FC ya Kenya.
Kadikilo ni beki wa kushoto alijiunga na Pamba Jiji FC akitokea Fountain Gate. Camara ni raia wa Gueinea ana miaka 24, yupo hapo kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Singida Black Stars. Khamis huyu aliwahi kucheza ndani ya Klabu ya Simba SC kwa sasa yupo Pamba Jiji FC.
Dennis Richard huyu ni mlinda mlango amepita KMC FC, JKT Tanzania. Henry Msabila ni mshambuliaji chipukizi ambaye alikuwa Kilombero Soccernet Academy. John Ben ni kiungo mshambuliaji raia wa Uganda. Alijiunga na Pamba Jiji FC akitokea Tabora United ambayo kwa sasa inaitwa TRA United.
Kikosi cha Simba SC vs Pamba Jiji FC
Langoni
Mahamadou Kassali. Huyu ni raia wa Mali mwenye umri wa miaka 29. Ni mlinda mlango ambaye alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Pamba Jiji FC ya Mwanza, Uwanja wa CCM Kirumba.
Mabeki
Shomari Kapombe, De Reuck, Nickson Kibabage na Ismael Toure ni mabeki wa Simba SC walikuwa kwenye doria ya ulinzi mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC.
Shomari Kapombe ni beki wa kulia katika kikosi cha Simba SC pia ni nahodha mwenye uzoefu mkubwa NBC Premier League. De Reuck ana miaka 30 ni raia wa Afrika Kusini huyu ni beki wa kati. Nickson Kibabage ni beki wa kushoto aliwahi kucheza Yanga SC ni raia wa Tanzania na Ismael Toure huyu ni raia wa Ivory Coast ana umri wa miaka 28 ni beki wa kati.
Viungo
Katika eneo la viungo dhidi ya Pamba Jiji FC ni Libasse Gueye, Ellie Mpanzu, Allasane Kante, Yusuph Kagoma na Clatous Chama walianza kwa Simba SC.
Libasse Gueye raia wa Senegel mwenye miaka 22, Ellie Mpanzu raia wa DRC Congo ana miaka 24,, Alasane Kante raia wa Senegel ana miaka 25, Yusuph Kagoma raia wa Tanzania ana miaka 29 na Clatous Chama raia wa Zambia mwenye miaka 34.
Mshambuliaji
Anicent Oura ndiye mchezaji aliyeshambulia katika mechi ya Pamba Jiji FC vs Simba SC. Jembe hili kutoka nchini Ivory Coast liliwavuruga Pamba Jiji FC kwa kupiga shuti moja ambalo lilisababisha goli.
Wachezaji wa akiba
Bashiri Salum, Anthony Mligo, Vedastus Masinde, Duchu, Hussen Abel, Naby Camara, Neo Maema, Hussen Mbegu,Semfuko na Morice.
SOMA HII: Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi/ Msimamo, matokeo


